Share
PUBLISHED ON December 13th, 2019

Mfumo wa Kieletroniki Wa Manunuzi, Uuzaji na Usafirishaji (NFLIP) Wazinduliwa

Mwenyekiti wa Makampuni ya Usafirishaji ya Simba,  Azim Dewj ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa mfumo unaowaunganisha wadau wa sekta ya Usafirisaji ”National Freight and Logistics Information Portal, akizungumza na wadau mbalimbali waliofika katika Uzinduzi huo ambao ni Mfumo ulioanzishwa na TPSF kwa ushirikiano na TMA una lengo la
kuwakutanisha watoa huduma za Usafirishaji na watafuta huduma kwa maana ya wenye mizigo.

Mwenyekiti wa Makampuni ya Usafirishaji ya Simba,Azim Dewj(Watatu toka kulia) Akizinduzia wa mfumo unaowaunganisha wadau wa sekta ya Usafirisaji ”National Freight and Logistics Information Portal.

Mwenyekiti wa Makampuni ya Usafirishaji ya Simba, Azim Dewj (Watatu toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja.

JUKWAA la Wafanyabiashara na wadau wa Usafirishaji kutoka Sekta Binafsi (TPSF) wamezindua mfumo wa kieletroniki wa manunuzi, uuzaji  na usafirishaji (NFLIP) utakaotumika katika nchini na nchi jirani.

Akizindua mfumo huo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kampuni ya Simba Group, Azim Dewji alisema kuwa, mfumo huo utawarahisishia wafanyabiashara kwa kupunguza gharama za usafirishaji kutoka eneo moja kwenda jingine.

‘’Mfumo huu utasaidia sana, badala ya mtu kutoka hapa kwenda Zambia au Kongo kununua mzigo, ukifika kule, utatafuta Hoteli, utatumia usafiri wa ndani ya nchi uliopo, mawasiliano ya ndani hiyo ni gharama, lakini ukitumia mtandao wa NFLIP itaokoa gharama nyingi kwani itafanya hayo yote kwa wakati mmoja, alisema Dewji.

Dewji alitoa mfano kuwa Bandari ya Tanzania ina uwezo wa kuhudumia nchi sita za Afrika Mashariki ambazo hazina Babdari, hivyo NFLIP itakuwa na uwezo wa kuhudumia nchi zote hizo kwa muda mfupi na kurahisisha muda wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Aidha alisema mfumo huu utazuia uongo unaonezwa na wafanyabiashara wa usafirishaji wa Kenya ambao wamekuwa wakiongopa kuwa ukitoa mzigo Bandari ya Tanzania unafika nchi jirani baada ya miezi mitatu.

‘’Sasa hivi katika biashara hakuna vita ya mtutu, kuna vita ya Kiuchumi, Wakenya wantabia ya kuwaongopea wafanyabiashara wa nchi jirani, kuwa bandari ya Tanzania inachelewesha mizigo, ili watumie Bandari ya Mombasa, sasa mfumo huu utaongeza kutokomeza uongo uo, alisema Dewji.

Aidha Dewji ameishukuru Serikali ya awamu ya tano ya Tanzania kwa usikivu kwani kila anapotoa kero za wafanyabiashara wamekuwa wakifanyia kazi na kutatua, na kuweka mazingira mazuri ya kufanyia biashara.

Pia Mfanyabiashara huyo mashuhuri hapa nchini, amewataka madereva wanaoenda nchi jirani wawe mabalozi wazuri wanapofika huko nje ya nchi, wawe wastaraabu, wasifanye mambo ya ovyo, kwani wakifanya hivyo wanaitukanisha jina la Tanzania jambo linaloweza kuchafua biashara ya usafirishaji.

Naye Mkurugenzi wa Miradi na uendeshaji wa TPSF Edward Furaha alisema, kupitia jukwaa la wafanyabiashara wamefanikiwa kuanzisha huduma hiyo ambayo itaokoa muda na gharama kwa wafanyabiasha na wadau wa usafirishaji nchini.

‘’Mfumo huu unawahusu wafanyabiashara, wasafirishaji na wenye bidhaa, hivyo ni teknolojia itakayowaweka pamoja watu wote hao kwa wakati mmoja na kwa gharama nafuu’’, alisema Furaha.

Aidha Mkurugenzi huyo alisema kutokana na ubora ulioonekana katika mfumo huo, TPSF ilipokea tuzo kutoka Trade Mark East Afrika ambayo ilijiridhisha na kuona mfumo huo utakuwa mkombozi kwa wadau wa usafirishaji na nchi jirani.

Source: Global Publishers

Disclaimer: The views and opinions expressed in this article are those of the authors and do not necessarily reflect the official policy or position of TradeMark Africa.