Mwenyekiti wa Makampuni ya Usafirishaji ya Simba, Azim Dewj ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa mfumo unaowaunganisha wadau wa sekta ya Usafirisaji ”National Freight and Logistics Information Portal, akizungumza na wadau mbalimbali waliofika katika Uzinduzi huo ambao ni Mfumo ulioanzishwa na TPSF kwa ushirikiano na TMA una lengo la kuwakutanisha watoa huduma za Usafirishaji na watafuta huduma kwa maana ya wenye mizigo. Mwenyekiti wa Makampuni ya Usafirishaji ya Simba,Azim Dewj(Watatu toka kulia) Akizinduzia wa mfumo unaowaunganisha wadau wa sekta ya Usafirisaji ”National Freight and Logistics Information Portal. Mwenyekiti wa Makampuni ya Usafirishaji ya Simba, Azim Dewj (Watatu toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja. JUKWAA la Wafanyabiashara na wadau wa Usafirishaji kutoka Sekta Binafsi (TPSF) wamezindua mfumo wa kieletroniki wa manunuzi, uuzaji na usafirishaji (NFLIP) utakaotumika katika nchini na nchi jirani. Akizindua mfumo huo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kampuni ya Simba Group, Azim Dewji alisema kuwa, mfumo huo utawarahisishia wafanyabiashara kwa kupunguza gharama za usafirishaji kutoka eneo moja kwenda jingine. ‘’Mfumo huu utasaidia sana, badala ya mtu kutoka hapa kwenda Zambia au Kongo kununua mzigo, ukifika kule, utatafuta Hoteli, utatumia usafiri wa ndani ya nchi uliopo, mawasiliano ya ndani hiyo ni gharama, lakini ukitumia mtandao wa NFLIP itaokoa gharama nyingi kwani itafanya hayo yote kwa wakati mmoja, alisema Dewji. Dewji alitoa mfano kuwa Bandari ya Tanzania ina uwezo wa kuhudumia nchi sita za Afrika Mashariki ambazo hazina Babdari, hivyo NFLIP itakuwa na uwezo wa kuhudumia nchi zote hizo kwa muda mfupi na kurahisisha muda wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Aidha alisema...
Mfumo wa Kieletroniki Wa Manunuzi, Uuzaji na Usafirishaji (NFLIP) Wazinduliwa
Posted on: December 13, 2019
Posted on: December 13, 2019