Kazi ya utekelezaji wa ujenzi wa Gati mpya kwa ajili ya kuhudumia Meli za magari (RoRo Berth) kwenye Bandari ya Dar es Salaam imefikia asilimia 50 na ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2019. Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema mbali na kukamilika kwa ujenzi wa Gati hiyo unaotarajiwa kukamilika katikati ya 2019, kazi ya kuboresha Gati namba 1 tayari ilishakamilishwa na Mkandarasi tangu tarehe 7 Disemba mwaka 2018. “Mkandarasi alikamilisha kazi ya ujenzi wa Gati namba 1 ambayo ilihusisha kuongeza eneo la kupakia na kupakua mizigo pamoja na kuongeza kina cha maji mpaka mita 14.5 na kazi kama hiyo kwenye Gati Namba 2 mpaka 4 ambayo inatarajiwa kukamilika na kukabidhiwa ifikapo mwezi Julai mwaka huu 2019,” amesema Kakoko. Mkurugenzi Mkuu amebainisha kwamba kwa upande wa ujenzi kwenye Gati namba 5 mpaka 7 kwa sasa Mkandarasi anaendelea na usanifu wa kina (detailed design) ambapo kazi ya ujenzi inatarajiwa kuanza mwezi Novemba 2019. Mradi wa uboreshaji Bandari ya Dar es Salaam (DMGP) unatekelezwa kwa awamu mbili ili kutoathiri uendeshaji wa shughuli za Bandari (port operations) wakati wa utekelezaji wake. Awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mradi inahusisha maboresho ya Gati namba 1-7 pamoja na Gati mpya kwa ajili ya Meli za magari. Gati hiyo mpya inajengwa kwenye eneo la Gerezani Creek ambapo TPA ilisaini mkataba na Mkandarasi M/s China Habour Engineering Company Limited kutoka nchini China tarehe 10 Juni 2017 kwa kipindi cha miaka mitatu huku gharama za Mradi zikikadiriwa kuwa ni Shilingi Bilioni 330. Awamu ya pili ya...
UJENZI GATI JIPYA LA MAGARI BANDARI YA DAR WAFIKIA ASILIMIA 50
Posted on: April 25, 2019
Posted on: April 25, 2019