Arusha. Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) limesaini mkataba wa makubaliano wa miaka mitano na taasisi ya Trade Mark East Africa (TMA) kutekeleza mradi wa kuondoa vikwazo kwa wafanyabiashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaoanza mwaka huu. Mkurugenzi Mtendaji wa EABC, Peter Mathuki amesema leo Jumatatu April 15, 2019 kuwa watashirikiana na Srikali za nchi za EAC kuona namna ya kuondoa vikwazo hivyo ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo maafisa wa Serikali wanaohusika kwenye maeneo ya mipakani. Amesema kiwango cha kufanya biashara baina ya nchi za EAC kipo chini ya asilimia 20 ukilinganisha na nchi za Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Sadc) ambapo ni asilimia 58 wakati nchi za Umoja wa Ulaya ni asilimia 68. “Lengo la mradi huu ni kuona namna ya kuinua kiwango cha biashara katika nchi zetu, mtakumbuka wakati wa mkutano wa Marais wa EAC uliofanyika hivi karibuni wote walisisitiza umuhimu wa hizi nchi kuongeza kiwango cha kufanya biashara miongoni mwetu ili wananchi waweze kunufaika,” amesema Mathuki. Amesema uamuzi wa TMA kushirikiana na EABC unaonyesha imani waliyonayo katika kusukuma ajenda ya EAC ya kuwawezesha wananchi kunufaika na jumuiya kwa kuvuka mipaka kwa ajili ya kuuza na kununua bidhaa mbalimbali. Mathuki amesema tayari vikwazo vya biashara 47 vimeshatatuliwa huku vikwazo 17 bado havijapatiwa ufumbuzi jambo ambalo linarudisha nyuma ufanisi wa kufanya biashara katika nchi hizo. Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa TMA anayeshughulikia Sekta Binafsi, Allan Ngugi amesema wamekua na ushirikiano na EABC tangu mwaka 2010 na uhusiano wao umekua mzuri hatua inayowapa nafasi...
Mkataba kuondoa vikwazo kwa wafanyabiashara EAC wasainiwa
Posted on: April 16, 2019
Posted on: April 16, 2019